Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wateketeza nyumba Mwanza

IliyopitaMoto Wa Kaskazini Wachochea Israel Kuchukua Hatua Kumaliza Mzozo.png Moto wateketeza nyumba Mwanza

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Mwanza limefanikiwa kuuzima moto uliozuka majira ya jioni katika nyumba iliyopo kata ya Nyakato wilayani Ilemela chanzo kikitajwa kuwa ni kulipuka kwa gesi.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mwanza Kamila Labani amesema moto huo ulizuka jana majira ya saa kumi jioni na kufanikiwa kuteketeza vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo huku hakuna mtu aliyepata madhara kutokana na moto huo kudhibitiwa haraka.

Katika hatua nyingine kaimu kamanda Kamila ametoa wito kwa wakazi wa jiji hilo la Mwanza kuhakikisha wanakuwa makini pindi wanapotumia majiko ya gesi na kuhakikisha wanafunga vizuri ili kujiepusha na madhara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live