Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wateketeza mabanda Soko Kuu la Mpanda, Tanzania

83596 Pic+soko Moto wateketeza mabanda Soko Kuu la Mpanda, Tanzania

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katavi. Zaidi  ya vibanda vitano vya soko kuu mjini Mpanda Mkoani Katavi, Tanzania, vimeteketea kwa moto ulioanza ghafla usiku wa kuamkia leo.

Shuhuda  wa tukio hilo, Ayoub Kassim amesema moto huo ulianza  ghafla  saa  sita  usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara zilizokuwemo kwenye vibanda hivyo.

“Moto  huo umesababishwa na hitilafu ya umeme,” amesema Kassim.

Hata hivyo, Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Katavi limewahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti moto huo uliokuwa ukisambaa kwa kasi.

Hadi  sasa bado haijafahamika thamani ya mali zilizoteketea katika tukio hilo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili.

Chanzo: mwananchi.co.tz