Moto umeteketeza chumba kimoja Cha mpangaji katika Mtaa wa Misewe, Kata ya Liwiti wilayani Ilala Dar es Salaam na kupelekea kifo cha mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na wiki Moja.
Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda inadaiwa Mama wa mtoto huyo alimuacha chumbani akiwa amelala na kwenda dukani Kwa ajili ya kutafuta Mahitaji muhimu, na alikuta chumba chake kikiteketea na mtoto akiwa ndani, licha ya majirani kujaribu kuokoa uhai wa mtoto huyo, jitihada hizo zilishindikana kutokana na mazingira kutokuwa rafiki.
Akizungumza na Wasafi Media Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Misewe, Abdallah Simbili amesema chanzo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambayo ilitokea ndani ya nyumba hiyo na kupelekea baadhi ya samani kushika moto.