Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wateketeza Nyumba ya Vyumba 12

IIIIIIII Moto wateketeza Nyumba ya Vyumba 12

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyumba moja yenye vyumba 12 katika mtaa wa Kiusa mjini Moshi imeteketea kwa moto alfajiri ya leo Mei 17, 2023 huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.

Shuhuda wa tukio hilo Glory Charles amesema alikuwa amelala katika mojawapo ya chumba na kusikia cheche za moto zikilipuka.

"Nilikuwa nimelala cheche zilinishtua na moto niliyaona ukiwa juu ya bati ukiwaka kuelekea upande wa jikoni nilipiga kelele za kuomba msaada na Kisha nikaenda Polisi ambao waliviambia wanakuja," amesema mwanadada huyo akibubujikwa na machozi.

Mmiliki wa nyumba hiyo Benjamin Abdi amesema waliwasiliana na Jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao wakiwataka wawe na subiri kidogo ambapo walifika baada ya dakika 30 na kufanikiwa kuzima moto huo.

Kwa upande wao Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro Eli Juma amesema walifika wakitokea wilayani Mwanga ambako walioenda kwa ajili ya kuzima moto ulipokuwa umewaka katika gari la gesi.

Thamani ya uharibifu huo inakadiriwa kuzidi milioni 20 kwani lilikuwa ni eneo ambalo biashara ya vinywaji baridi na pombe imekuwa ikifanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live