Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto waliza wafanyabiashara soko la Sabasaba Dodoma, vibanda vyateketea

90259 MOTO+PIC Moto waliza wafanyabiashara soko la Sabasaba Dodoma, vibanda vyateketea

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara wadogo maarufu ‘machinga’ vilivyopo  nje ya soko la Sabasaba Jijini Dodoma nchini Tanzania, vimeteketea kwa moto unaodaiwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Desemba 29, 2019 eneo la tukio, mmoja wa wafanyabiashara hao waliounguliwa na vibanda hivyo, Adam Makumburu amesema kwenye banda lake alikuwa akiuza simu za  na vifaa vingine ambavyo vyote vimeteketea kwa moto.

Makumburu amesema bidhaa hizo zina thamani ya zaidi ya Sh25 milioni na kwamba  hakufanikiwa kuokoa chochote.

Kwa mujibu wa Makumburu, moto huo ulianza kuwaka saa moja asubuhi na taarifa ya tukio hilo aliipata kutoka kwa wafanyabiashara wenzake.

Mwenyekiti wa soko hilo, Eduad Ndahani alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo amesema hawezi kuzungumzia akisema bado ana machungu ya kuteketea kwa kibanda chake.

Hata hivyo,  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini hapa, lilifika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima moto huo uliokuwa ukisambaa kwa kasi kabla ya kusababisha madhara zaidi katika soko hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz