Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moshi yatangaza idadi ya vijiji, vitongoji vya uchaguzi serikali za mitaa

75631 Moshi+pic

Fri, 13 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania imetangaza majina na mipaka ya vijiji 157 na vitongoji 700 vitakavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 24, 2019.

Akitoa tangazo hilo leo Ijumaa Septemba 13, 2019  msimamizi wa uchaguzi huo, Juma Tukosa amesema halmashauri hiyo ina Vitongoji 700, vijiji 157, kata 32 na majimbo mawili ya uchaguzi.

Tukosa ametumia nafasi hiyo kuwataka watendaji wa kata kuwa mabalozi wazuri wa kufikisha taarifa mbalimbali za uchaguzi ikiwa ni pamoja na elimu ya uraia kwa kutoa matangazo kwa njia mbalimbali katika maeneo yao.

"Ni haki ya wananchi kupata taarifa zote za uchaguzi kwa wakati na kwa uwazi mkubwa ili kufanya uamuzi sahihi katika kuchagua viongozi wanaowataka, hivyo ni jukumu lenu watendaji kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi," amesema Tukosa.

Akizungumza Katibu wa NCCR-Mageuzi Jimbo la Vunjo, Mathew Temu amewataka wananchi kujiepusha na matukio ya vurugu na wasikubali kudhulumiwa haki yao na mtu yeyote.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz