Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moshi yafanya vizuri matumizi ruzuku ya elimu

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa kusimamia matumizi ya fedha za ruzuku ya elimu kwa shule za msingi.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jumatano Oktoba 2,2019 na mkuu wa Takukuru mkoa Kilimanjaro, Holle Makungu baada ya kufanya ufuatiliaji katika shule 10 kati ya 35 zilizopo ndani ya Manispaa.

“Ili kuziba pengo la michango ya elimu, Serikali imekuwa ikipeleka capitation grants (ruzuku) ya Sh10,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka, ili kuwapunguzia wazazi gharama,” alisema Makungu.

Kwa mujibu wa Makungu, Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, ilianza kutekeleza ahadi yake ya kutoa elimu bure kwa shule za Serikali.

“Tulifuatilia katika kipindi cha kati ya Januari 2019 hadi Juni 2019 katika shule 10 kati ya 35 za Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na kubaini zimesimamiwa vizuri,” alisema Makungu.

Alizitaja shule za msingi zilizohusika katika ufuatiliaji huo kuwa ni Magereza, Soweto, Jamhuri, JK. Nyerere, Sokoine, Muungano, Kiborlon, Msaranga, Mawenzi na Mwenge.

Pia Soma

Advertisement
“Tunawapongeza wote walioshiriki katika usimamizi wa fedha hizo. Ni rai yetu kwa wazazi na wananchi wote wataendelea kuunga mkono serikali katika mpango wake huu,” alisema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi alipoulizwa anajisikiaje Halmashauri yake kupongezwa na Takukuru, alisema hilo limewapa faraja watumishi.

Chanzo: mwananchi.co.tz