Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moro watoa Sh bil 1.4 za mikopo ya vikundi

4a2207ced1368b12756f030a4971552c Moro watoa Sh bil 1.4 za mikopo ya vikundi

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 1.4 kutoka kwenye vyanzo vyake

vya ndani vya mapato kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuanzia mwaka 2015 hadi sasa.

Kati ya fedha hizo kiasi cha Sh milioni 677.6 zimetolewa kwa vikundi 297 vya wanawake , Sh milioni 647.7 kwa vikundi 194 vya vijana na Sh milioni 86.9 kwa vikundi 23 vya watu wenye ulemavu.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, Enedy Mwanakatwe , alisema hayo kwenye taarifa iliyohusu mikopo kwa makundi hayo wakati wa kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani Desemba Mosi mwaka huu ambapo kimkoa ilifanyika kwenye Manispaa hiyo.

Mwanakatwe , alisema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Manispaa imetoa mkopo usiokuwa na riba wa jumla ya Sh milioni 560.2 kwa vikundi 59 vya wanawake, vikundi 39 vya vijana na vikundi 10 vya watu wenye ulemavu .

"Mkopo huu umetolewa kwa lengo la kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato na kuinuka kiuchumi," alisema Mwanakatwe.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro, alisema mkopo kwa vikundi vyote 106 kati ya 108 umekwishatolewa , na vikundi viwili vilivyokuwa vimebakia ni vya vijana ambao wanajishughulisha na usafirishaji wa abiria vya Bomsate na Tunaweza Mindu.

Mwanakatwe alisema vikundi viwili hivyo vimekopeshwa pikipiki 37 zenye thamani ya Sh milioni 88.01 na kukabidhiwa Desemba Mosi katika kilele cha siku ya Ukimwi duniani na kimkoa iliyofanyika Manispaa ya Morogoro.

Pamoja na hayo, alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao waliokabidhiwa pikipiki hizo kwa wale wenye tabia hatarishi ambazo zina athiri jamii ikiwa ni pamoja na kuutumia usafiri huo katika uhalifu na kuwarubini watoto wa kike hasa wanafunzi kuacha tabia hizo mara moja.

Naye, Mwenyekiti wa Kikundi cha Bomsate , Awadhi Hamis alisema kikundi hicho kina wanachama 57 na lengo la kikundi ni kumwezesha mwanachama kumiliki pikipiki yake , kujenga nyumba pamoja na kuwa na duka la vifaa vya pikikipi la Kikundi.

Chanzo: habarileo.co.tz