Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mongella: Ajali ya Mv Bukoba ni kumbukumbu mbaya yenye funzo

58893 Mvpic

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Taifa likiadhimisha miaka 23 tangu kuzama kwa meli ya Mv Bukoba Mei 21, 1996, Serikali imesema tukio hilo litaendelea kuwa miongoni mwa kumbukumbu mbaya kutokana na kuangamiza maisha ya mamia ya Watanzania kwa wakati mmoja.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 800 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea kilomita chache kutoka bandari ya Mwanza.

Akizungumza leo Jumanne Mei 21, 2019 katika ibada maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo katika eneo la makaburi ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema fundisho lililotokana na ajali hiyo limeongeza umakini na usimamizi wa Serikali kwenye usafiri majini.

“Licha ya kuongeza usimamizi kuzuia ajali zinazoepukika, Serikali pia imewekeza kwenye sekta ya usafirishaji kwenye sekta ya usafiri wa majini ikiwemo ukarabati na ujenzi wa meli mpya,” amesema Mongella.

Amesema uwekezaji pia unaendelea katika usafirishaji kwa njia ya anga, reli na barabara.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Eric Hamissi ametaja miongoni mwa uwekezaji unafanywa na Serikali katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji kuwa ni ukarabati wa meli za Mv Victoria na kwa gharama ya Sh22 bilioni na Mv Butiama unaokarabatiwa kwa Sh3 bilioni.

Pia Soma

“Serikali pia unatekeleza mradi wa ujenzi wa chelezo na meli mpya utakaosafirisha abiria 1, 200 na tani 400 ya mizigo kati miji ya Bukoba na Mwanza kwa gharama ya zaidi ya Sh89 bilioni,” amesema Hamissi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz