Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnaokereka na foleni za Dar hamieni vijijini - RC Chalamila

Chalamila: Viongozi Wa Dini Muiombee Serikali Mnaokereka na foleni za Dar hamieni vijijini - RC Chalamila

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka wanaokerwa na foleni ya Jiji hili wahamie kijijini kwakuwa moja ya sifa ya Dar ni foleni inayosababishwa na wingi wa Watu na wanaoisababisha ni wanaonunua magari na wale wanaotoka Mikoa mingine kila kukicha kuja Dar es salaam.

Chalamila amesema hayo leo December 19,2023 wakati akiongea kwenye mkutano wake na Wamiliki wa Bar, Night Clubs na Grocery “Tumshukuru Rais wetu Mh. Samia kwa jinsi alivyokazana kuifungua Nchi, Nchi inafunguka sana, Nchi ikifunguliwa mnapata Wadau wanaopenda kunywa bia na vinywaji vingine na mnapata Watu, nyie mnakumbuka kabla ya Mh. Rais hajaingia madarakani baadhi ya Watu walikimbia Nchi na kwenda kuishi Ughaibuni lakini Rais Samia alipoingia akasema wote warudi tujenge Nchi pamoja”

“Jana nimenukuliwa nikisema yoyote anayedhani Dar es salaam inamkera sana ahamie kijijini hili nilikuwa namaanisha sio kwamba nazungumza kwa utani yaani Mimi utani ndio huwa maanisho hilohilo, naomba niliweke sawa, Tanzania imeumbwa na Mungu yapo maeneo yamepewa baridi kali, joto kali na joto la wastani, ukikuta hali ya kwenye joto kali inakusumbua hamia kwenye joto la wastani au kwenye baridi, moja ya sifa ya Mkoa wa Dar ni kuwa na joto na kama unakuja Dar unaanza kulilalamikia joto maana yake unatakiwa uondoke uende kwenye baridi, hoja ya pili Mtu anaweza kusimama akisema ‘Dar foleni sana Serikali haijafanya kazi kupunguza foleni’, kuna vijiji vingi havina foleni hamia kwenye kijiji ambacho hakina foleni”

“Aliyesababisha foleni Dar ni Mimi na wewe tulionunua gari, Serikali imewezesha Watu kununua magari na Rais anajenga mabarabara, fly over kila kukicha lakini kila akijenga fly over kinakuwa kivutio cha wengine kutoka kijijini kuja Mjini, sifa ya pili ya Dar ni population ipo juu na ndio raha ya Dar”

“Hata tungejenga mabarabara makubwa kwa namna gani yataendelea kuwa kivutio kwa wengine wataendelea kujaa, ndio maana tunasema sifa zisiwe sababu ya kulalamika kwasababu moja ya Mkoa wa Tanzania uliopata mabilioni ya fedha ya ujenzi wa miundombinu ni Dar, tumejenga fly over lakini foleni bado zipo vilevile kwasababu bado Watu wananunua magari wanahamia Dar”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live