Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuanzia sasa ni marufuku kubadili matumizi ya eneo kwa kutumia vitambaa vya mabango na badala yake ni lazima uitwe mkutano wa wananchi wa mtaa mzima.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuanzia sasa ni marufuku kubadili matumizi ya eneo kwa kutumia vitambaa vya mabango na badala yake ni lazima uitwe mkutano wa wananchi wa mtaa mzima. Waziri Silaa amesema hayo wakati alipofanya ziara katika maeneo ya Oysterbay na Msasani jijini Dar es salaam akiongozana na viongozi wakuu wa Wizara mbapo alikuta baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wameanza kujenga vyumba vya kupangisha vya biashara kinyume na matumizi ambayo ni makazi.