Nyumba zaidi ya 100 katika Kata ya Viwanja Sitini na Kata ya Mbasa, Halmashauri ya Mji Ifakara, Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro, zimethiriwa kutokana na kuzingirwa ana maji ya Mto Lumemo yanayosababishwa na mvua kubwa za masika na kusababisha Mtu mmoja kusombwa na maji.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kilombero, Haji Muduluka amethibitisha kuwa hadi sasa zaidi ya wananchi 40 wameokolewa, na jitihada za kuokoa wengine zinaendelea.
Baadhi ya Wananchi walioathirika wameeleza kuwa wamepoteza chakula na makazi yao kutokana na mafuriko hayo.
Aidha, wamesema wanaomba kwa dhati jitihada zaidi za uokoaji kufanywa ili kunusuru maisha yao, hasa kwa ukuzingatia mvua izo zinaendelea kunyesha.