Mwanamke mmoja amefariki na mwingine kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba dhahabu katika kijiji cha Merenga Kata ya Nyansurura wilaya ya Serengeti.
Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Desemba 30, 2021 ambapo kumekuwa na matukio kadhaa ya vifo vya namna hiyo katika eneo hilo. Mwaka 2017 watu watatu wengine walikufa katika shimo hilo.
Mwaka 2019 alikufa mtu mmoja, Desemba 20 mwaka huu alikufa Kibwabwa Nyaisawa na wenzake wawili Nyahiri Nyahiri na Wesiko Makenge kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dk Vicent Mashinji amesema,hakuwa na taarifa. Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Merenga Moses Ryoba akiongea na Mwananchi amemtaja aliyekufa kuwa ni Maria Okama (40)mkazi wa Kitongoji cha Mafyeko na majeruhi ni Bhoke Marwa(38)mkazi wa Kitongoji cha Senta kijijini hapo
"Shimo hilo lililokuwa linamilikiwa na Rubeni Mtenga mkazi wa Tarime baada ya kusababisha mauaji mwaka 2017 na kuibuka mgogoro na mwenye shamba lilifungwa,na Desemba 29 akina mama hao walianza kuchimba sijajua waliruhusiwa na nani,"amesema.