Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmoja afariki kwa kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo

75031 Kifusipic

Tue, 10 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mtu mmoja amefariki, wanane kunusurika na mmoja kutojulikana alipo baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya dhahabu wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza leo Jumanne Septemba 10, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati wachimbaji wadogo wa dhahabu wakiwa kwenye shughuli zao za uchimbaji.

“Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wapatao kumi waliingia kwenye shimo na ukiangalia ilikuwa usiku lakini baadae kifusi katika njia ya kuingilia kiliwafunika."

‘’Watu wanane wameokolewa wakiwa hai lakini bahati mbaya watu wawili kati ya hao kumi walioingia, mmoja amefariki dunia na mwingine jitihada za kujua alipo zinaendelea,“amesema.

Kamanda Murilo amesema bado uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

“Kuna sababu mbalimbali kwenye machimbo,  ukitokea mtetemo wowote ardhi inaweza kuporomoka na mvua zinanyesha kidogo, lakini bado tunachunguza hasa nini kimesababisha, " amesema.

Pia Soma

Advertisement
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz