Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlinzi wa shule auawa akidaiwa kuiba jiko

PANGA Mlinzi wa shule auawa akidaiwa kuiba jiko

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndugu wa mlinzi wa shule ya Wasichana Korogwe, Bw.Frank Mhina, aliyefariki baada ya kushambuliwa, kwa madai ya wizi wa jiko la gesi la shule hiyo wamegoma kuuzika mwili wa ndugu yao hadi waliosababisha umauti wa mlinzi huyo wakamatwe.

Kufuatia tukio hilo, tumemtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, lakini simu yake imepokelewa na msaidizi wake ambaye amedai kuwa yupo kwenye kazi maalum.

Akizungumza nasi, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji wa Korogwe, Vasco Mwambipile, amethibitisha kumpokea mlinzi huyo, ambaye kwa taarifa za awali zilisema alikuwa ameshambuliwa, lakini alifariki wakati akiandaliwa kwa ajili ya Rufaa ya kwenda hospitali ya Mkoa ya Bombo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live