Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa mkoa wa Tabora awatembelea majeruhi wa ajali Nzega

Mkuu Wa Mkoa Wa Tabora Awatembelea Majeruhi Wa Ajali Nzega Mkuu wa mkoa wa Tabora awatembelea majeruhi wa ajali Nzega

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi.Dkt.Batilda Burian amewatembelea majeruhi wa Ajali ya Basi iliyotokea Wilayani Nzega Mkoani Tabora ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mji Nzega na Hospitali ya Rufaa Nkinga na kuwafikishia salamu za pole kutoka kwa Mhe.Rais.Samia Suluhu Hassan na kuwapa posho ya kujikimu pamoja na Asali lita moja kila mmoja kwa matumizi ya Chakula na Tiba.

“Mpaka sasa kati ya majeruhi 60 waliobaki hospitali ni 19 na wote wanaendelea vizuri. Wawili wapo Bugando nao wanaendelea vizuri. Miili kumi na tatu tayari imekwisha tambuliwa bado miili 5 ambayo tunaendelea kuwatafuta ndugu na jamaa zao, ikumbukwe kuwa basi la Alpha lilikuwa linatoka Mwanza siku hiyo ya tarehe 21 Oktoba,2023 kwenda Dar-es-Salaam.Tunaomba tufuatilie ndugu na jamaa zetu ili miili yote iweze kuchukuliwa na kusitiriwa,” amesema Mkuu wa Mkoa

“Tunaendelea kutoa pole kwa ndugu na jamaa wa wote waliofariki katika ajali hiyo mbaya” Mhe.Balozi.Dkt.Batilda Burian , Mkuu wa Mkoa wa Tabora .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live