Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa Wilaya afunga madanguro, yaharibu Wanafunzi (+Video)

Makahaba 2 Mkuu wa Wilaya afunga madanguro, yaharibu Wanafunzi

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash amefunga nyumba nne ambazo Wanawake wanatumia kuuza miili yao (Madanguro) katika Kijiji cha Kwaruhombo Kata ya Mbwewe Wilayani humo baada ya Wanafunzi 51 wa Shule ya Msingi ya Kwaruhombo kubainika wanafanyiana vitendo vya kingono ikiwemo kuingizana vijiti sehemu za siri na walipohojiwa wakasema wanajifunza tabia hizo kutoka kwenye Madanguro.

DC Okashi ametembelea eneo hilo na kufanya ukaguzi ambapo amesema licha ya kuyafunga Madanguro hayo pia watawachukulia hatua Wamiliki wa nyumba hizo ambapo wanaendelea pia na msako kubaini nyumba nyingine zinazotumika kufanya biashara hiyo.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Chalinze, Atunagile Chisunga amesema hatua zilizochukuliwa kwa Wanafunzi ni kuwafanyia msaada wa kisaikolojia pamoja na kuwaunganisha na huduma za afya pia wamefanya mkutano na Wazazi Shuleni kuwaeleza madhara ya vitendo vya ukatili na wajibu wa Wazazi na Walezi kuwalinda Watoto kwenye Familia ambapo amesema Jamii inaogopa kutoa taarifa kwa kuhofia kurogwa “Kuna machimbo ya dhahabu katika eneo hilo nahisi inaweza kuwa kisababishi cha uwepo wa Madanguro”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live