Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa Wilaya aahidi kukamiliika kwa madarasa

3aedd88aad206ef01f19c97461393804 Mkuu wa Wilaya aahidi kukamiliika kwa madarasa

Sun, 3 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge amemuhakikishia Mbunge wa Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki ukamilishwaji wa vyumba vya madarasa mpaka kufikia Januari mwakani ili kuwawezesha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuanza masomo kama ilivyopangwa.

“Tunaendelea na ujenzi kwa kushirikiana na wananchi, mkurugenzi na watumishi wote wa halmashauri kwenye kuhakikisha mikakati inapangwa ili ifikapo mwezi Januari mwakani ujenzi wa madarasa uwe umeshakamilika,” amesema Kaminyoge.

Aidha, Kaminyoge amesema kuwa halmshauri hiyo ina shule mbili mpya ambazo zikipata usajili zitasaidia kutatua tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa.

Naye, Mbunge wa Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki amewataka watumishi wa halmashauri kuhakikisha kasi ya ujenzi inaongezeka ili ifikapo Januari mwakani madarasa yawe yamekamilika kwakuwa muda uliobakia ni mdogo.

Chanzo: habarileo.co.tz