Moshi. Agizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), la kutaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rombo, Margareth John awajibishwe, linaingia katika orodha ya kauli kali za viongozi dhidi ya utumishi wake.
LAAC imeingia katika orodha hiyo ya kuonyesha shaka dhidi ya utendaji wake baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally pia kuonyesha wasiwasi naye.
Alipotafutwa kwa simu jana kuulizwa kuhusu ongezeko la kauli dhidi yake, Margareth alipokea na kusikiliza swali la mwandishi na alipoulizwa anazungumziaje maagizo hayo ya LAAC ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu, alikata simu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo pia hakupatikana kuzungumzia suala hilo na alipopigiwa simu, alirudisha ujumbe kuwa atafutwe baadae.
Juzi, mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Vedasto Ngombale aliagiza mamlaka zinazohusika kumchukulia hatua za kinidhamu DED huyo kwa kushindwa kumudu nafasi yake.
Kamati hiyo pia iliagiza kushitakiwa kwa watumishi wa wilaya hiyo waliotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusika na ubadhirifu wa fedha.
Pia Soma
- Simulizi ya Mwanamke Mtanzania dereva wa malori aliyetekwa DRC
- Mambo saba ziara ya Dk Bashiru Dar es Salaam
- Mbowe amwombea ruhusa Sugu kwa mkewe
“Ukifuatilia kama dokezo lilianzia kwa mkuu wa idara husika, huoni dokezo. Kwa hiyo kuna ujanja ujanja unafanyika mpaka watu wanajilipa,”alisema.
Kwa undani wa Habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi, Septemba 1, 2019