Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi aingia darasani kufundisha

Screenshot 2021 03 17 At 10.11.04 660x400.png Mkurugenzi aingia darasani kufundisha

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mnasi Haji amejiwekea utaratibu wa kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi hadi saa moja na dakika 40 kupita darasani katika Shule mbalimbali zilizopo Makao Makuu ya Halmashauri hiyo na kuwafundisha Wanafunzi wa darasa la saba, anaifanya hii kila siku kabla ya kuendelea na majukumu mengine.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mnasi Haji amejiwekea utaratibu wa kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi hadi saa moja na dakika 40 kupita darasani katika Shule mbalimbali zilizopo Makao Makuu ya Halmashauri hiyo na kuwafundisha Wanafunzi wa darasa la saba, anaifanya hii kila siku kabla ya kuendelea na majukumu mengine. Amesema anafanya hivyo kwakuwa yeye Kitaaluma ni Mwalimu na Ualimu upo kwenye damu, licha ya kuwa na uwezo wa kufundisha masomo mengi kwa sasa hufundisha zaidi Hisabati, hizi picha ni akiwa Shule ya Msingi Nyerere Ileje.

Chanzo: millardayo.com