Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi aimamisha watatu kupisha uchunguzi

Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Ya Jiji La Tanga Said Majaliwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Said Majaliwa

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: Mwananchi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Said Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili za kukiuka miongozo ya Serikali ya ujenzi.

Katika taarifa yake iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini, Mussa Labani usiku wa Desemba 27,2023 imeeleza kuwa watumishi hao wanatuhumiwa kukiuka miongozo ya Serikali ya ujenzi wa majengo ya mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa kuongeza gharama tofauti na maelekezo ya wizara na kuruhusu kuingiwa.

Taaifa hiyo iliwataja watumishi waliosimamishwa kazi kwaajili ya kupisha uchunguzi huo kuwa ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Miundombinu, Issa Mchezo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiomoni, Fredirick Lubangulila na Mhandisi wa Majengo, Baraka Noni.

Chanzo: Mwananchi