Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi Iringa azungumzia mchakato wa kumng’oa meya

98080 Pic+meya Mkurugenzi Iringa azungumzia mchakato wa kumng’oa meya

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Iringa, Hamid Njovu amemtaka meya, Alex Kimbe kuzisoma na kuzielewa kanuni zinazoongoza halmashauri hiyo badala ya kulalamika kuwa anaonewa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Njovu alieleza kuwa madiwani 19 walimwandikia barua Februari 27, mwaka huu kumwomba aitishe mkutano maalumu na ajenda ikiwa kupiga kura ya kukosa imani na mwenyekiti wao wa baraza, ambaye ni meya.

Alisema jukumu lake kama meya ilikuwa kuzipitia kanuni ili kuona kama madiwani wenzake wamekiuka taratibu na jukumu lake ni kujibu tuhuma hizo kwa kufika kwenye kikao na kutoa utetezi wake.

Mkurugenzi huyo alimwandikia barua meya huyo akimpa siku tano za kujitetea kutokana na kukabiliwa na tuhuma nne ikiwamo ya matumizi mabaya ya ofisi kwa kufanya maamuzi bila kuzingatia kanuni zinazoongoza manispaa hiyo.

Tuhuma ya pili inayomkabili meya huyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za ofisi ikiwamo kutumia gari kwa matumizi yake binafsi.

Meya huyo pia anakabiliwa na tuhuma ya mwenendo mbaya au ukosefu wa adabu na nyingine ikiwa kujihusisha na masuala ya rushwa.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Hata hivyo, Kimbe amepinga mchakato huo na kueleza kuwa atajibu barua ya mkurugenzi kupinga mchakato huo na kuwa yupo tayari kwenda mahakamani.

“Wale waliomchagua ndio wataona kama utetezi wake una mashiko basi watambakiza kwenye nafasi yake na kama wakiona hauna mantiki yoyote watamwondoa madarakani kwani tuhuma zinazomkabili ni za kimaadili na kiuongozi na wala si kijinai,” alieleza.

Njovu alisema kanuni ya 83 ya kupiga kura ya kumuondoa madarakani inaruhusu theluthi mbili ya waliohudhuria kikao hicho kumuondoa madarakani meya kwa kupiga kura, kwa hiyo majibu yote atayapata kwenye kikao cha baraza la madiwani, ambapo madiwani wote 28 wanatazamiwa kupiga kura kuamua hatima yake.

“Theluthi mbili ya madiwani wakipiga kura kumkataa mstahiki meya itabidi aachie ngazi, ingawa ana nafasi ya kukata rufaa kama atakuwa anaamini mchakato wa kumwondoa haukuwa sahihi au kupeleka malalamiko kwa waziri mwenye dhamana na masuala ya serikali za mitaa.

“Utaratibu ambao ulitumika kumweka madarakani ni kanuni hizi hizi za mwaka 2015 na ndio utakaotumika katika mchakato wa kumuondoa madarakani,” alieleza.

Njovu alieleza kuwa kifungu cha 5(2) cha kanuni zinazoongoza halmashauri za miji kinamwelekeza mkurugenzi akipokea barua ya maombi kama hayo jambo la kwanza ni kuhakikisha mambo mawili yameambatanishwa, moja likiwa ni orodha ya madiwani ambao wanataka kufanya mchakato.

Pili idadi yao itoshe theluthi mbili ya madiwani wote wa Manispaa ya Iringa, ambao awali walikuwa 28 na karibuni wametoka wawili na kubakia 26.

Kutokana na hali hiyo akidi ambayo inatosha kuitisha mkutano wa baraza la madiwani wa manispaa ya Iringa ni 19.

Njovu aliongeza kuwa jambo jingine wanalopaswa kufanya madiwani hao ni kuambatanisha tuhuma ambazo wamemuelekezea mstahiki meya.

lisema baada ya kupokea barua hiyo jukumu lake ni kumtaarifu Meya na kumuambatanishia tuhuma hizo ili yeye ajibu ndani ya siku tano na hizo ndio hatua za kwanza ambazo anadai amezifanya na anasubiri majibu.

“Hoja iliyopo hapa ni kuwa kuna madiwani wanamtuhumu diwani mwenzao na wametumia kanuni ambazo zinaeleza utaratibu, kwa hiyo meya anapaswa kuelewa jambo hilo,” alieleza mkurugenzi huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz