Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkurugenzi Duwasa aonja joto ya jiwe

257c3e09ecea85500859888ace4c6b38 Mkurugenzi Duwasa aonja joto ya jiwe

Fri, 11 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), David Palangyo amekuwa wa kwanza kuonja joto ya jiwe baada ya kusimamishwa kazi na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.

Aweso amemsimamishakazi Mkurugenzi huyo na kumuagiza Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga kumbadilisha kituo cha kazi Palangyo.

Aweso ambaye ameapishwa jana na Rais John Magufuli amesema haridhishwi na utendaji kazi Palangyo kwa kile alichodai kuwa Jiji la Dodoma linahitaji mtendaji mwenye kasi zaidi na kwamba Palangyo asubiri kupangiwa kazi nyingine.

"Najua kaka yangu umefanya kazi kubwa, hata hivyo lazima tuwe wakweli kwamba Dodoma tunahitaji kasi zaidi kwa kuwa macho ya viongozi yanatazama hapa, sitakuwa mpole naomba utupishe utapangiwa majukumu mengine baadaye," amesema Aweso.

Kiongozi huyo amesema ni wakati wa watumishi wazembe kukaa mguu sawa na ikibidi waanze kupisha wenyewe na kusisitiza kuwa atawapa ushirikiano mkubwa watumishi wote kuanzia ngazi ya chini hadi juu.

Aidha Waziri Aweso amewaonya watumishi wa Duwasa watakaoanza kukwamisha kazi ya mkurugenzi atakayeteuliwa, “hao ndio watakuwa wa kwanza kuondoka kabla ya huyo aliyepewa jukumu hilo.”

Chanzo: habarileo.co.tz