Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkojo wa sungura sasa lulu

56736 Pic+sungura.png

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Baadhi ya wakulima wameanza kugeuza changamoto kuwa fursa kwa kubuni njia mbadala kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao mashambani.

Badala ya kutumia viuatilifu vinavyodaiwa kutoua wadudu, wakulima sasa wanatumia mkojo wa sungura baada ya kubaini una uwezo wa kudhibiti visumbufu.

Hayo yalibainika juzi wakati wa ziara ya kutembelea mashamba ya wakulima wa mbogamboga wilaya za Nyamagana na Magu iliyoandaliwa na asasi ya Tanzania Hotculture Assocition (Taha) inayosaidia wakulima kulima kwa tija.

“Ninanyunyiza mkojo wa sungura shambani kuua wadudu katika miche 3,000 ya mapapai, nimefanikiwa tangu nianze kutumia mbinu hii miezi mitatu iliyopita,” alisema Bernard Makachira, mkulima wa Nyamagana. “Sasa navuna mapapai 300 kwa wiki ndoto yangu ni kufikisha miche 10,000. Kilio ni ukosefu wa huduma za ugani,” alisema.

Pia, kilio cha kukosa huduma ya ugani kilitolewa na mkulima wa mbogamboga anayetumia kilimo cha bustani nyumba (Green house), Peter Ngongoseke, mkazi wa kijiji cha Masanza One wilayani Magu, aliyesema amelazimika kuajiri maofisa ugani kutoka Kenya.

Kuhusu kutumia mkojo wa sungura, mtaalamu wa kilimo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Wenseslaus Joseph alisema baadhi ya njia mbadala hazijafanyiwa utafiti kuthibitishwa kitaalamu lakini zimeonyesha mafanikio.

Pia Soma

Akifungua mkutano wa wadau wa pamba jijini Mwanza Aprili, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa alikiri kuwapo kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya viuatilifu kukosa ubora.

Chanzo: mwananchi.co.tz