Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkoa wa Mara watajwa kinara wa kulima na kutumia bangi

27525 Mara+pic TanzaniaWeb

Sat, 17 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imewasilisha bungeni taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2017 ikionyesha kuwa Mkoa wa Mara unaongoza kwa kulima na kutumia bangi kati ya mikoa minane.

Taarifa hiyo ilitolewa jana bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama na kuitaja mikoa mingine kuwa ni Arusha, Njombe, Tanga, Simiyu, Rukwa, Geita na Morogoro.

Hata hivyo, alisema kiasi cha bangi kilichokamatwa kilipungua kutoka tani 68.23 kwa mwaka 2016 na kufikia tani 52.19 kwa mwaka 2017.

Kuhusu ukamataji wa mirungi, Mhagama alisema uliongezeka kutoka tani 21.6 kwa mwaka 2016 hadi kufikia tani 67.8 mwaka 2017 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara tatu.

Hata hivyo, alisema idadi ya watuhumiwa waliokamatwa kutokana na mirungi ilipungua kutoka 2,397 mwaka 2016 hadi 1,797 mwaka 2017 na hiyo ilichangiwa na tuhumiwa wengi kukamatwa na kiasi kikubwa cha mirungi na baadhi ya mirungi kukamatwa bila wahusika kuwepo baada ya kuitekeleza.

Mhagama alisema kiasi cha cocaine kilichokamatwa kilipungua kutoka kilo 18.52 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 4.143 mwaka 2017 na hata watuhuhumiwa waliokamatwa kwa wakijihusisha na mihadarati hiyo walipungua kutoka 263 kwa mwaka 2016 na kufikia 243 kwa mwaka 2017.

Alisema kumekuwa na ongezeko la dawa za kulevya aina ya heroine zilizokamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya baada ya kuimarisha udhibiti wa dawa zinazopita mipakani na hivyo kupunguza uingizaji wake nchini.

Alisema heroine ambayo ilikamatwa nchini katika mwaka 2016 ilikuwa kilo 42.26 ikilinganishwa na kilo 185.557 zilizokamatwa 2017 ikiwa ni mara nne zaidi na kiasi hicho ambacho ni kikubwa kuwahi kukamatwa nchini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Alisema pia idadi ya watuhumiwa waliokamatwa wakijihusisha na heroine iliongezeka kutoka watu 716 kwa mwaka 2016 hadi kufikia 1,005 mwaka 2017.

Mhagana alisema mashamba ya mirungi ya ukubwa wa ekari 64.5 yaliteketezwa katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.



Chanzo: mwananchi.co.tz