Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkizaa marufuku kuachana - RC Queen Sendika

Sendigaaaaa Web Mkizaa marufuku kuachana - RC Queen Sendika

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amesema wenza wenye Watoto hawatakiwi kuachana badala yake wanatakiwa kuwa pamoja kulea Watoto.

Amewaagiza Viongozi wa Serikali za Vijiji na Kata Mkoani hapo kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya dola Vijana watakaobainika kushindwa kulea Watoto na kuzitelekeza Familia zao.

"Ninatoa maelekezo kuanzia Serikali ya Kijiji kwamba kijana yeyote atakayeletwa ofisini kwa kushindwa kutunza mtoto tutamshughulikia. Umetia mimba, lea mtoto wako na ni marufuku kuachana.

"Huyo uliye naye ulipatana naye siku ya kwanza, kwa hiyo utajijua mwenyewe kwa sababu kama ni masawe ni ya kwako na kama ni kiazi ni cha kwako, kamatana nacho kwa faida ya watoto wako.

"Sio siku mbili unajifanya mwanamke huyu humtaki, wewe siku ya kwanza unamchukua ziwa limesimama sasa hivi ananyonyesha ziwa haliwezi kusimama tena, wewe vipi? Kaeni mlee watoto wenu kwa sababu tunawategemea kesho," amesema Queen Sendiga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live