Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenda: Hakuna wanaume walevi Rombo

Prof Mkenda Till Mkenda: Hakuna wanaume walevi Rombo

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rombo mkoa wa Kilimajaro amesema amepanga kukutana na wanaume wote wa Rombo wanaoishi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao utawajumuisha Mbunge wa Rombo, Madiwani na wana Rombo umepangwa kufanyika Ukumbi wa Kardinali Adams Msimbazi Senta Ilala, agenda ikiwa kujadili maendeleo ya Jimbo la Rombo.

Profesa Mkenda amesema mkutano huo utakaofanyika Mei 5, 2024,si wa kwanza ni mwendelezo wa mikutano aliyofanya Marehemu Bazil Mramba aliyewahi kuwa Mbunge wa Rombo.

Profesa Mkenda amesema Wanaume wa Rombo wamesambaa mataifa mbalimbali wakifanya kazi wanamchango mkubwa kwa wilaya yao wapenda maendeleo na hata maduka mengi ya Kariakoo maneno ya" Chako ni Chako" Dodoma wengi hapo ni watu kutoka Rombo.

"Kuhusu kauli zinazosema kuwa wanaume wa Rombo ni walevi wa kutupwa wanaume wa Rombo wamesambaa maeneo mbalimbali na kuna kauli inasema ukienda sehemu usipowakuta Warombo ondoka haraka hivyo wana mchango mkubwa kwa uchumi wa wilaya kama suala ya kunywa wanakunywa baada ya kazi" Amesema Prf.Mkenda

Na ameongeza kwa kusema suala la ulevi Rombo ni jambo linalokuzwa na halina uhalisia kabisa wanaume wa Rombo sio walevi ni wanaume wanaojitambua na wachapakazi.

Akijibu changamoto ya maji jimboni kwake Profesa Mkenda amesema Wilaya ya Rombo inakabiliwa na shida kubwa ambayo inachangiwa na uhaba wa vyanzo vya maji hivyo katika mkutano huo wa mei 5, atazungumzia suluhu ya tatizo la maji katika Jimbo la Rombo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live