Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa mwenyekiti abakwa na kuuawa Kagera

Mke Wa Mwenyekiti Khadija Mke wa mwenyekiti abakwa na kuuawa Kagera

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Khadija Ismail (29) amebakwa na kisha kuuawa kwa kupigwa kwa kitu butu kichwani na kijana aliyetambulika kwa  jina la Paschal Kagwa (22) aliyekuwa akiishi naye.

Tukio hilo la kinyama limeripotiwa kutokea jana Jumatatu, Februari 13, 2023 majira ya jioni.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema kuwa kijana anayetuhumiwa kumbaka mama huyo alikuwa akiishi nyumbani kwa mwenyekiti baada ya kupewa hifadhi. "Aliishi nao nyumba moja lakini sio ndugu yao alipewa hifadhi tu." 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live