Juma Said Mfaume Mkazi wa Mbagala Mlandizi mkoani Pwani amefariki baada ya kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa Kampuni ya OYA Microcredit waliokuwa wamefika nyumbani kwake majira ya Alfajiri siku ya Jumanne tarehe 08 Oktoba 2024.
Mke wa Juma aitwaye Khadija alikopa mara ya kwanza kupitia kampuni hiyo akawa ameshindwa kurejesha kiasi cha 60,000/= wakakaa na kujadiliana na kampuni husika huku wakimshauri kuchukua mkopo mpya ili aweze kulipa kiasi kilichobaki.
Kutokana na maelezo ya Khadija alianza kufanya marejesho lakini alipata changamoto ya kurejesha kutokana na changamoto za kibiashara.
Siku ya tarehe nane majira ya saa kumi wafanyakazi hao walifika nyumbani kwake na kumgongea dirishani wakimwita mkewe lakini Juma hakufungua mpaka ulipofika wakati wa Sala ya Subh/Alfajir alipotoka nje ndipo pakawa na ubishani juu ya marejesho hayo huku akiwataka wamsubiri mkewe arejee.
Wahusika waliendelea kushinikiza kutaka kuingia ndani ili waweze kuchukua baadhi ya vitu kufidia mkopo huo lakini mhusika alipokataa wakaanza kuzozana wakitaka kumpiga ndipo kwenye kubishana mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo akaokota kigongo na kumpiga eneo shingoni na akaanguka.
Baada ya kuanguka walimbeba kwenye gari na kuondoka naye baadae taarifa zikatoka kupitia uongozi wa kitongoji kuwa Juma yupo hospitali baada ya kupigwa na baadae alipoteza maisha.