Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (MOI) hii leo Februari 28, 2023 imetoa taarifa mpya juu ya majeruhi aliyeburuzwa kwenye ajali ya mwendoskasi wiki iliyopita.
Taarifa hiyo imetolewa na Mejeja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi akieleza pia kwamba mke na ndugu wengine wamejitokeza.
Taarifa hiyo imeeleza; “Tunapenda kuufahamisha Umma kwamba majeruhi pekee wa ajali ya mwendokasi aliyekuwa amesalia MOI ametambulika, jina lake ni ndugu Osam Milanzi, mkazi wa Manzese Midizini (Dar).
“Utambuzi umefanywa na mke wake Bi Isha Mohamed pamoja na mdogo wa Ndugu Osam, bwana Shaban Milanzi.
“Afya ya ndugu Osam imeimarika sana kutokana na kazi kubwa ambayo imefanywa na madaktari, wauguzi pamoja na watumishe wengine wa MOI.”
MOI tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari pamoja na Watanzania wote wenye mapenzi mema ambao wameshirikiana nasi kutangaza habari za kuwatafuta ndugu wa Bwana Osam.”