Mwili wa Mfanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha Christian Temu umeshindwa kuzikwa katika Kata ya Moshono Mkoani Arusha licha ya taratibu zote za mazishi kukamilika ikiwemo kaburi kuchimbwa baada ya Mke wa Marehemu aitwaye Yasinta Kilawe, kwenda Mahakamani na kuweka zuio la Mumewe kutozikwa kwa madai ya kutokushirikishwa kwenye taratibu za mazishi.
Mwanamke huyo alipeleka maombi hayo madogo na kuweka zuio hilo Mahakamani kupitia Mawakili wake hadi hapo pande zote mbili zitakaposikilizwa na kufikiwa mwafaka.
Imeripotiwa kuwa katika msiba huo kila kitu kilikuwa kimeandaliwa lakini Waombolezaji kutoka sehemu mbalimbali wamelazimika kuondoka hadi watakapotangaziwa siku nyingine ya maziko.