Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke asiyeona amtafuta mumewe

Fri, 12 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Title: Mke asiyeona amtafuta mumewe

Summary: Mathias amepotea siku ya tisa sasa na haijulikani alipo huku mkewe ambaye ni mlemavu wa macho akihaha kumtafuta.

 

Shani Awadhi mwananchi

[email protected]

Dar es salaam, Zikiwa zimepita siku 9 bila kuonekana, Mathias Simon (63) mkazi wa Tabora ambaye ni mgonjwa na anapoteza fahamu, anatafutwa na mkewe Sophia Hassan.

Sophia amesema mume wake ametoweka nyumbani kwa dada yake Temeke kwa Azizi Ally tangu Oktoba 2 saa mbili asubuhi akiwa amevalia shati la mistari na koti la suti.

“Mimi ni mgonjwa wa macho tumekuja kutibiwa kwa dada wa mume wangu lakini sikuweza kumuona wakati anatoka nyumbani kwa sababu sioni,”amesema Sophia.

 “Naomba Mungu anipe nguvu niweze kuupita mtihani huu nitumie dawa nipone niweze kumtafuta mume wangu kwani bado nina imani kwamba nitamuona,” amesema Sophia.

Dada wa Mathias, Modesta Simon anasema siku ambayo Mathias alipotea, hakuwepo nyumbani alienda kwenye biashara zake za kila siku na alivyorudi nyumbani hakumkuta Mathias.

“Nilipo jaribu kuuliza kwa majirani walisema hawajamuona tulishirikiana kumtafuta na tukaona twende polisi kutoa taarifa,” anasema Modesta.

Amesema tumejaribu kumtafuta hadi Muhimbili kwa sababu huwa tunampeleka kupata matibabu lakini hatujafanikiwa kumuona.

“Hatujui anakula nini na kinachotupa wasiwasi ni mgonjwa, watoto wake wanashindwa kuendelea na masomo kutokana kutojua nini hatima ya baba yao,” amesema Modesta.

Amesema kilichobakia sasa ni kuomba tu Mungu tumuone akiwa salama kwani tumemtafuta bila matumaini ya kumuona hasa kwa kuwa haujui mkoa wa Dar es salaam vizuri.

“Kwa sasa hali ya maisha hapa nyumbani imekuwa ngumu kwa sababu biashara zangu zimesimama,” amesema Modesta.

Kwa atakayefanikiwa kumuona atoe taarifa kituo chochote cha Polisi au watumie namba 0684930027

 

Chanzo: mwananchi.co.tz