Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke adaiwa kutafuta wauaji waliomuua mumewe

Wauajii Web Mke adaiwa kutafuta wauaji waliomuua mumewe

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: eatv.tv

Washtakiwa watano akiwemo mke wa marehemu ambaye inadaiwa alipanga njama za kumuua mume wake aitwaye Mange Washa na aliwalipa wauaji wawili kiasi cha shilingi laki nane, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza na kusomewa shtaka moja la mauaji.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba, Ndeko Dustan Ndeko, washtakiwa hao watano wamesomewa shtaka la mauaji namba 12 la mwaka huu na Mwendesha Mashtaka wa serikali Robert Mwanakatwe, na hawakutakiwa kujibu chochote kufuatia mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza keai hiyo 

Washtakiwa hao ni pamoja na Makoye Lusana, Masunga Mange, Pascal Mange, Hoka Mazuri ambae ni mke wa marehemu pamoja na Shija Salum ambao inadaiwa mnamo Desemba Mosi mwaka huu walipanga njama na kumuua Mange Washa kwa madai kuwa alimfukuza nyumbani mtoto wake anayedaiwa kuwa ni mwizi.

Inaelezwa kitendo hicho cha kumfukuza mtoto wake huyo kilimkera mke wake ambaye ni mshtakiwa namba nne Hoka Mazuri na kulazimika kupanga njama za kumuua mume wake huyo kwa kushirikiana na watoto wake wawili na watu wengine wawili aliowalipa shilingi laki nane, ambao walifanikiwa kumkata shingo na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kupelekea mwanaume huyo kupoteza maisha.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kwimba Ndeko Dastan Ndeko akaiahirisha keai hiyo hadi tarehe 28 ya mwezi huu itakapotajwa tena huku washtakiwa wote watano wapelekwa rumande katika gereza la wilaya hiyo kufuatia kesi yao kutokuwa na dhamana.

Chanzo: eatv.tv