Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke, Mume waliosombwa na Maji kuzikwa kesho Kilolo

D518adfb75c250e10b7cc878429be2ca Mke, Mume waliosombwa na Maji kuzikwa kesho Kilolo

Sun, 7 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAIMU Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (Taliri) Kanda ya Kati, Dk Harun Chawala na mkewe Dk Neema Mwasanganga waliofariki dunia usiku wa jana baada ya gari lao kusombwa na maji wakati wakivuka daraja la Shaaban Robert mjini Mpwapwa, watazikwa kesho mkoani Iringa.

Akizungumza na Mtandao huu, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk Sulemain Serera ambaye yupo eneo la tukio alisema miili ya wanandoa hao imeagwa leo Jumapili Machi 7,2021 nyumbani kwao Taliri wilayani humo.

“Tumeaga leo na miili imesafirishwa kwenda nyumbani kwa mwanaume (Dk Chawala) Wilayani Kilolo mkoani Iringa,” amesema.

Amesema mazishi ya wanandoa hao yatafanyika kesho nyumbani kwa Dk Chawala Wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Tukio hilo lilitokea juzi saa mbili usiku wakati gari lao aina ya Nissan X-trail lenye usajili namba T483 BRR kusombwa na maji kwenye daraja hilo lililopo meta chache kutoka ilipo ofisi ya mkuu wa wilaya.

Chanzo: www.habarileo.co.tz