Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkazi Tabora aigonga treni, afariki dunia

Tue, 8 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Shaban Juma, mkazi wa Igalula Wilaya ya Uyui Mkoa wa Tabora ameigonga treni na kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Emmanuel Nley ameeleza hayo leo Jumatatu Januari 7, 2019.

Amesema tukio hilo limetokea jana saa 2 asubuhi na kwamba marehemu alikuwa akitembea kwa miguu kwenye njia ya treni na kuigonga.

Amebainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hispitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora, Kitete na kwamba uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.



Chanzo: mwananchi.co.tz