Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkazi Dar azama Bonde la Jangwani

83620 Pic+jangwani Mkazi Dar azama Bonde la Jangwani

Thu, 14 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuwa waangalifu ili wasipatwe na madhara kufuatia mvua zinazoendelea.

Mjema ametoa angalizo hilo leo wakati akishiriki zoezi la uokoaji wa mwili wa mkazi mmoja wa jiji hilo aliyezama katika Bonde la Jangwani wakati akiwa katika shughuli zake za kuokota chupa za plastiki.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa jitihada za kutafuta mwili wa mtu huyo hazijazaa matunda ila vikosi vya uokoaji vinaendelea kuutafuta.

“Tusiwe tunasema haya maji ni kidogo mimi ni mzoefu, unaweza ukaingiza mguu tope likakukamata maji yakiendelea kuja huna ujanja, kitakachotokea ni kama kilichomtokea huyu mwenzetu,”

“Nafahamu wengi mnajua kuogelea, nisingependa kama kiongozi wa serikali kuona tunapoteza mtu mwingine, hivyo naomba msiingie tuviache vyombo vya uokoaji vifanye kazi hiyo,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz