Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi wa maji kuanza kazi Monduli

Maji Monduli Mkandarasi wa maji kuanza kazi Monduli

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na changamoto ya ukame iliyoikumba wilaya ya Monduli, Serikali imesema iko kwenye hatua za mwisho za kumpata mkandarasi kwa ajili ya kupeleka maji wilayani humo.

Wananchi wa Monduli wanasota kusaka maji kutokana na hali ya ukame iliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, iliyoikumba wilaya hiyo.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa juma Jijini Arusha na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akizungumza baada ya ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira (AUWSA).

Kamati hiyo ilikagua mradi mkubwa wa maji wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru (ASUWSDP).

Waziri Aweso alisema Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kumpata mkandarasi ambapo maji hayo yatatolewa kwenye mradi huo wa ASUWSDP unaogharimu zaidi ya Sh520 bilioni.

Alisema mradi huo ambao uko katika hatua za mwisho unatarajiwa kuzalisha maji lita milioni 200, huku mahitaji ya jiji la Arusha yakiwa lita milioni 109

Alisema lazima maji hayo yapelekwe maeneo ya pembezoni ikiwemo Monduli ambayo kwa sasa ina uhaba wa maji.

“Maelekezo ambayo tunayatoa kwa mamlaka hii ni kuhakikisha maeneo ya pembezoni yanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama, lakini haya maji ni toshelevu yafike maeneo mengine,”alisema

“Tumeona eneo la Monduli kumekuwa na changamoto, maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, ni kwamba maji haya yafike Monduli na tupo hatua za mwisho kabisa za kumpata mkandarasi kuhakikisha maji haya yanafika Monduli,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Justine Rujomba,alisema mradi huo ambao unatekelezwa kwa mchango wa serikali na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live