Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi atupwa jela kwa kuidanganya halmashauri

Jelaaaaaa Halmashaurii Mkandarasi atupwa jela kwa kuidanganya halmashauri

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani au kulipa faini ya shilingi Milioni moja mkandarasi baada ya kukutwa na hatia ya kuidanganya halmashauri.

Mkandarasi Hans Bariki Makenya ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Lucky Construction Limited ya Dar Es Salaam alifikishwa Mahakamani na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Makete kwa kesi ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wake ambaye ni halmashauri  kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Makete Chilomwa Bitulo amesema Mtuhumiwa aliandaa nyaraka ya uongo kuwa amejenga tanki la mradi wa maji Matamba lenye ukubwa wa ujazo QMita 100 ilihali amejenga QMita 72.5 na kuomba kulipwa fedha za Qmita 100 kinyume na sheria ambapo kesi yake ilifikishwa Mahakamani tarehe 6 February 2023.

Hakimu wa Mahakama hiyo Ivan Msaki amesema mshtakiwa amekiri kosa lake na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi Milioni moja ambapo

amekubali kulipa faini na kuachwa huru lakini hata hivyo fedha alizoombaa kulipwa hakufanikiwa baada ya kosa lake kugundulika mapema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live