Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi apewa wiki 2 ujenzi nyumba ya RC, DC

D3a6e45db2489183b4ac57ed1aeb242d Mkandarasi apewa wiki 2 ujenzi nyumba ya RC, DC

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa siku 14 kwa mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya Dodoma na ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kukamilisha ujenzi na ukarabati huo kwa wakati.

Dk Mahenge alitoa agizo hilo jijini hapa baada ya kufanya ziara kukagua maendeleo ya miradi hiyo ya ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya ya Dodoma na ukarabati wa nyumba ya mkuu wa mkoa Dodoma.

Pia mkuu wa mkoa alifanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru na ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala wa wilaya ya Chamwino, katika mkoa huo ili pia kuona thamani ya fedha iliyotumika.

Dk Mahenge alisema mkandarasi wa ujenzi wa nyumba ya DC na mkarabati wa nyumba ya RC hawataongezewa muda, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanaongeza nguvu kazi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

“Wakandarasi wa miradi hii wanatakiwa kuongeza kasi kwa kuongeza nguvu kazi ya watu ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na hakuna uwezekano wa kuongezewa muda,” alisema.

Dk Mahenge alitoa muda huo utakaokamilika Agosti 3, mwaka huu kutokana na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba ya DC na ukarabati wa nyumba ya RC. Kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Dk Mahenge alitoa mwito kwa mkandarasi Suma JKT kuhakikisha ifikapo Agosti 23, mwaka huu anakamilisha ujenzi wa hospitali hiyo na kuikabidhi rasmi.

Alisema hospitali hiyo inahitajika kwa ajili ya kupanua huduma za afya mkoani humo, hivyo kukamilika kwa wakati kutasaidia kuongeza huduma hiyo muhimu kwa watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla wake.

Chanzo: habarileo.co.tz