Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi aliyesimamishwa arejeshwa

Wed, 14 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imemrudisha mkandarasi, kampuni ya Overseas Infrastructure Pvt Ltd ya India ambaye alikuwa amesimamishwa katika mradi wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze ili amalizie kazi yake ifikapo Desemba mwaka huu.

Hata hivyo mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete ametia shaka majibu ya Serikali kwamba haiwezekani mradi huo kukamilika Desemba kwani kazi bado ni kubwa.

Naibu Waziri wa Maji,  Jumaa Aweso ameliambia Bunge kuwa katika kutekeleza mradi huo awamu ya tatu, Serikali iliamua kumrejesha mkandarasi huyo kwa kuwa kuajiri mkandarasi mpya ingechukua muda zaidi.

"Mkandarasi huyo amepewa masharti mapya yatakayohakikisha kazi inafanyika kwa kasi ambapo masharti hayo ni pamoja na kuhakikisha analeta fedha za kuwalipa makandarasi wadogo aliowaajiri," amesema Aweso.

Aweso ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Ridhiwan ambaye alitaka kujua Serikali imeshachukua hatua gani ili kusaidia kuondoa tatizo kubwa la maji katika halmashauri ya Chalinze akihoji ni lini  mradi huo unatarajiwa kukamilika.

Naibu Waziri amesema kwa makubaliano yao, mkandarasi anatarajia kukamilisha mradi huo ifikapo Desemba 2018 na Wizara inaendelea kuhakikisha mkandarasi huyo anasimamiwa hatua kwa hatua na akizembea hatua zitachukuliwa dhidi yake.



Chanzo: mwananchi.co.tz