Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi akimbia mradi Geita

Barabara Mkandarasi akimbia mradi Geita

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkandarasi wa Kampuni ya Palemon Construction Ltd ya jijini Mwanza ‘amekimbia’ mradi wa ujenzi wa barabara ya Molinge mjini Geita yenye urefu wa mita 300, Meneja wa Wakala Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Geita, Mhandisi Japherson Nnko amedai mbele za waandishi wa habari.

Ujenzi wa barabara hiyo ulipangwa kuanza Juni 6 hadi Novemba 3, 2022 kwa gharama ya Sh milioni 230 hata hivyo, mkandarasi huyo ameondoka bila kukamilisha mradi huo.

“Mradi haujaenda kama ulivyotarajiwa kwa sababu mpaka sasa muda umeisha kabisa, kwa maana ya muda tupo kama asilimia 115 lakini kazi iliyofanyika ni chini ya asilimia 10,” amesema.

“Sisi masharti yote ya mkataba kama mwajiri tumeshakamilisha ikiwemo malipo ya awali, na ameshalipwa takribani Sh milioni 21 kama malipo ya awali kumsaidia kwa ajili ya kufanya kazi.”

Amesema ameshaandikiwa barua ya onyo na sasa anakatwa asilimia 0.01 kila siku anavyochelewa kukamilisha mradi na endapo makato yatafikia asilimia 10 atavunjiwa mkataba kwa mjibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live