Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane anayemsomesha mwanaye kwa kuuza mkaa atamani kuacha biashara hiyo

40686 Mjanepic Mjane anayemsomesha mwanaye kwa kuuza mkaa atamani kuacha biashara hiyo

Fri, 8 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mjane anayemsomesha chuo mwanaye kwa kuuza mkaa amesema anatamani kuachana na biashara hiyo kwa sababu huwa anasikitishwa na uharibifu wa mazingira unaofanyika katika maeneo anayochukua mkaa.

Mjane huyo Bahati Masebu ameyasema hayo leo Alhamisi Februari 7, 2019 katika mahojiano maalumu kabla ya kuanza kwa mdahalo wa tatu wa Mwananchi Jukwaa la Fikra lililobeba mada ya Mkaa, Uchumi na Mazingira yetu.

Bahati amesema wakati wote anaofanya biashara hiyo amekuwa akijisikia vibaya jinsi miti inavyokatwa na mazingira kuharibika katika baadhi ya maeneo lakini hana namna anayoweza kufanya ili kumudu gharama za kimaisha.

"Biashara hii imenitoa mbali, imenisaidia kulea na kusomesha watoto wangu katika ngazi mbalimbali za kielimu pamoja na kununua viwanja vitatu," amesema Bahati.

Lakini wakati akizungumza hayo Bahati amesema katika kipindi chote cha ufanyaji biashara hiyo amekuwa akizingatia na kufuata sheria za uuzaji mkaa kwa kuchukua vibali vitakavyomruhusu kufanya usafirishaji.

"Usipokuwa na kibali unaweza kupata hasara kwa kutozeshwa faini kubwa na wakati mwingine kunyang'anywa mzigo wako," amesema Bahati.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri kwenye mdahalo huo unaorushwa moja kwa moja na kituo cha ITV pamoja na MCL Digital



Chanzo: mwananchi.co.tz