Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjamzito auawa kikatili kwa kuchinjwa, wauaji nao wauawa

Mauaji Mdhd Mjamzito auawa kikatili kwa kuchinjwa, wauaji nao wauawa

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mwenye ujauzito wa miezi saba aliyetambuliwa kwa jina la Renata Elias (27), ameuawa kikatili na mtoto wake wa kambo kwa kuchinjwa shingo huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na tamaa ya mali.

Tukio hilo lililotokea usiku wa Februari 17, 2023 linadaiwa kufanywa na vijana wawili ambapo mmoja ni mtoto wa mume wa mwanamke huyo na kwamba baada ya kufanya mauaji hayo nao waliuawa na wananchi wenye hasira kali.

Katika tukio hilo, pia baba wa familia hiyo aliyetajwa kwa jina la Msafiri Renatus alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu ubavuni na kichwani na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Geita kwa matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba aliyetekeleza tukio hilo la kinyama anaitwa Jackson Msafiri (25) ambaye alikuwa na rafiki yake.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Magembe ameitembelea familia iliyoathirika na tukio hilo kulaani vikali huku akitoa pole kwa familia na kuwashukuru wananchi kwa kuonyesha umoja uliofanikisha kumnusuru Msafiri na kumwahisha hospitali baada ya kujeruhiwa.

“Sisi kama serikali tumefika kuwapa pole kwenye jambo hili zito na baya ambalo kwa binadamu yeyote mwenye akili anaona ni tukio baya la kufedhesha utu wa binadamu watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutenda.

“Kilichofanywa ni kitendo kibaya sana, niseme tu nawashukuru wananchi kwa kujitokeza mliposikia na ushirikiano huu uendelee ili kudhibiti matukio ya aina hii,” amesema Magembe.

Mihayo Renatus ambaye ni kaka mkubwa wa Msafiri, amezungumzia tukio hilo akisema majira ya saa 2 usiku, mtoto mkubwa wa Msafiri akiwa na kijana mwenzake walifika nyumbani na kugonga kisha kufunguliwa geti na kuingia ndani kuangalia TV na baada ya muda mfupi walitekeleza mauaji hayo baada ya mwanamke huyo kuingia bafuni kuoga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Safia Jongo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu yake ya mkononi kutopokelewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live