Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjamzito akanyagwa na tembo na kuvunjika mguu

Mjamzito Na Tembo Na Mjamzito akanyagwa na tembo na kuvunjika mguu

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mjamzito anayefahamika kwa jila la Anna Michael (47) mkazi wa kata ya Dumbeta wilaya ya Hanang mkoani Manyara, amekatika mguu wa kulia kiasi cha kutenganishwa na mwili wake, baada ya kukanyagwa mguu huo na tembo wakati akimuokoa mtoto wake asiuawe na kundi la tembo nje ya nyumba yake wilayani humo.

Anna akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara, amesema tembo alimkanyaga mguu na ukakatika na kutengana na mwili hapo hapo eneo la tukio.

Aidha, Anna ameiomba Serikali imsaidie mguu wa bandia pamoja na mtaji wa biashara ili aweze kuacha kufanya kazi ya kupasua kokoto kutokana na hali yake ya sasa ya ulemavu. #GADITVUPDATES

Chanzo: www.tanzaniaweb.live