Dodoma. Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura)Dodoma, Geoffrey Mkinga amesema ujenzi wa miundombinu unakabiliwa na changamoto ya ujenzi holela katika jiji hilo.
Akizungumza na Mwananchi kuhusiana na ujenzi wa mtandao wa barabara katika jiji la Dodoma jana, Mkinga alisema kwa sasa mtandao wa barabara hauko kwenye hali nzuri kutokana na halmashauri ya jiji kupima na kugawa viwanja bila kufungua barabara za maeneo hayo.
“Na ndiyo maana utakuta kuna makorongo yanayopitisha maji ya mvua lakini hakuna sehemu maalum ya kuyapeleka maji hayo na hata kama ukisema uyapeleke mahali fulani utajikuta umeyaelekeza kwenye nyumba ya mtu,” alisema.
Mkinga alisema wanachokifanya sasa ni kutafuta mhandisi msaidizi ili afanye usanifu kwenye makorongo yote yanayopitisha maji ya mvua na watakapoyatambua watayaombea bajeti kwa ajili ya kuyajenga na kusafirisha maji hayo.
“Jiji la Dodoma lina jumla ya kilomita 846 za barabara ambazo zimeshafunguliwa na zaidi ya kilomita 564 ambazo bado hazijafunguliwa na zipo kwenye makazi ya watu.”
“Hizo ni baadhi ya kilomita za barabara ambazo zinajulikana, lakini kuna zaidi ya kilomita 120 zinazojumlisha barabara za mzunguko pamoja na zile zilizopo katika mji wa Serikali,” alisema.
Pia Soma
- KUTOKA LONDON: Tunapofiwa na tunaowapenda twajifunza nini?
- Uchoraji wa Tattoo unaweza kukunyima fursa hizi
- Uhusiano kati ya Damu na Tabia
- Namna bora ya kutunza afya ya mtoto nyumbani