Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitungi ya gesi ilivyolipuka Tabata "moto ulienea Mtaa mzima" (+video)

Video Archive
Sat, 3 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Kutoka Tabata Savanna, Dar es salaam usiku wa kuamkia leo imetokea ajali ya moto ambayo imesababisha duka la Shayo kuteketea, Mashuhuda wanasema zipo taarifa kuwa baada ya Shayo kupata taarifa za duka lake kuteketea alipoteza fahamu na kukimbizwa Hospitali.

Pembeni ya duka la Shayo kuna Shule ya Chekechea ya Destiny ambayo pia imeungua kwa sehemu kubwa huku baadhi ya nyumba zilizopo jirani zikipata madhara———“hakuna taarifa za vifo ila kuna majeruhi”

Mashuhuda wanasema Watu walipata taharuki mtaani baada ya moto huo kuambatana na vishindo vikali vilivyosababishwa na kulipuka kwa mitungi ya gesi ambayo ilikuwa inauzwa dukani kwa shayo———“mwanzoni tulifikiri Majambazi yamevamia mtaani”

“Chanzo tunahisi labda mitungi ya gesi imegongana kwasababu anaiweka kwenye jua baadaye anairudisha ndani au Mke wake amesahau kuzima vizuri jiko cheche ikaruka na kushika kitu ikawa moto”———Mama Shayo, Shuhuda

Chanzo: millardayo.com