Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitambo michache yakamisha ujenzi wa barabara Mirerani

Mitambo Mererani Mitambo michache yakamisha ujenzi wa barabara Mirerani

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Kasi ndogo ya Mkandarasi Riso Business holding LTD anayejenga barabara yenye urefu wa kilomita 0.5 kwa kiwango cha lami katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, yawakwaza wananchi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni hiyo, Emmanuel amesema mkataba wa ujenzi unawataka kumaliza ujenzi huo kwa muda wa miezi sita.

Wambura amesema walianza ujenzi Novemba 10 mwaka 2022 ambapo walitakiwa kujenga kwa kuweka tabaka tatu ikiwemo vifusi, udongo uliochanganywa na lami na lami yenyewe.

Amesema kikwazo kikubwa kinachofanya washindwe kumaliza ujenzi huo kwa wakati, ni uchaze wa mitambo waliyonayo kwani vinatumika katika miradi miwili, ukiwemo ule wa ujenzi wa barabara nyingine ya urefu wa kilomita 1.5 iliyopo Orkesumet.

"Kule makao Makuu ya Wilaya ya Simanjiro, mji mdogo wa Orkesumet, pia tunajenga barabara nyingine ya lami kwa kutumia baadhi ya vyombo vyetu hivyo inatupasa kujenga kule na huku," amesema.

Awali baadhi ya wakazi wa mji huo mdogo, waliiambia Mwananchi Digitital kuwa kusuasua kwa ujenzi barabara hiyo ya nusu kilomita, kunakwamisha shughuli za maendeleo ya kiuchumi kwa wilaya lakini pia kwa mtu mmoja mmoja.

Barabara hiyo iliyoanza kujengwa mwaka jana, imetumia muda mrefu kujengwa hali inayosababisha baadhi ya watu kushindwa kuitumia na hivyo kusababisha hasara kwao.

Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo Isack Lema akizungumza leo jumamosi Juni 3 amesema barabara hiyo inategemewa na watu wengi ikiwemo wafanyabiashara mbalimbali na jamii kwa ujumla hivyo mkandarasi aimalize.

“Wafanyabiashara wameathirika kwani baadhi ya magari yanashindwa kupita ili kuweka mafuta, wachomea vyuma, maduka, sokoni na wengineo wameathirika mno,” amesema Lema.

Amesema ni bora mkandarasi huyo angehakikisha ana fedha mkononi ndipo aanze kujenga barabara kwa muda husika na siyo kama anavyofanya sasa anaijenga taratibu mno.

Mkazi wa kata ya Endiamtu, Sokota Mbuya amesema mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo hana uwezo kwani ni kipande hakifiki hata kilomita moja ila ameshindwa kumaliza kwa muda mrefu.

“Tunamtaka aimalize haraka kwani vumbi lililopo ni kero na wanaokaa pembeni ya barabara hiyo wanaweza kupata ugonjwa wa kifua kikuu kwa sababu ya uzembe wa mtu mmoja,” amesema Mbuya.

Chanzo: Mwananchi