Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misungwi wajivunia ongezeko la wanaopima kwa hiari

5b37ead2f025d0b79d24f8b06ae3d636 Misungwi wajivunia ongezeko la wanaopima kwa hiari

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

LICHA ya kwamba hakuna tukio lolote lililofanyika katika kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Dunia (TB), Machi24, kutokana na kifo cha Rais wa awamu ya tano, Dk John Magufuli, Hospitali ya Misungwi jijini Mwanza inajivunia ongezeko la wagonjwa wanaojitokeza kupima afya kwa hiari.

Upimaji huo unafanyika kupitia Mradi wa miaka mitano wa Boresha (2016 hadi 2021) unaotekelezwa wilayani humo na Shirika lisilola kiserikali la masuala ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na TB la AGPAHI (-Ariel Glaser Pediatric Aids Health Care Initiative) kwa kushirikiana na serikali kupitia Wizaya ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto.

Mratibu wa wa masuala ya Ukimwi wa Wilaya, Regina David aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki kwamba, kupitia Boresha, shirika hilo limekua likiwajengea uwezo watoa huduma na wale wanoishi na VVU pamoja na TB ili kuhamasisha kila mgonjwa anayetembelea Hospitali hiyo kupima magonjwa hayo (VVU na TB).

"Wote walioshiriki mafunzo hayo hukaa kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) wanapoanzia wagonjwa wote na kuwashawishi wote kupima VVU hata kama shida zao ni nyingine. Baada ya kupima VVU, wale wanaoonekana kuwa na dalili za TB hupima mardhi hayo pia," alisema Mratibu.

Alisema ni kwa utaratibu huo wagonjwa wamekuwa wakijitokeza kwa wingi na kujua hali ya afya zao ambapo wanaogundulika kuambukizwa huanza matibabu mara moja, hatua inayopunguza maambukizi mapya kwani kila mgonjwa hufundishwa namna ya kuwakinga wenzake katika familia na jamii kwa ujumla.

Mtumiaji wa matibabu hayo, Mariam Joseph, anayetarajia kumaliza dozi yake (TB) mwezi ujao, alisema ugonjwa huo unatibika kwani sasa anaendelea vizuri ikilinganishwa na alipoanza matibabu.

Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kupima afya zao hata kama hawajaona dalili ili kupata matibabu kwa wakati, kwa wale watakaogundulika kuambukizwa.

Akizungumzi hali ilivyokua kabla ya mradi wa Boresha, Daktari katika kitengo cha HIV na TB, Sumbuo Kullay alisema wagonjwa wengi walikua wakijitokeza wakiwa tayari katika hatua mbaya na hivyo kuyafanya matibabu kuwa magumu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz