Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miradi ya maji inayosimamiwa na halmashauri ni shidaa

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema miradi mingi ya maji inayosimamiwa na halmashauri inakuwa na shida nyingi tofauti na ile inayosimamiwa na wakandarasi wengine.

Ameyasema hayo leo Aprili 29, 2019 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Halamashauri ya Busekelo wakati Rais John Magufuli alipokuwa akifungua kipande cha barabara chenye kilomita 10 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mbeya.

Amesema licha ya kuwa Busekelo wana shida ya maji kwa muda mrefu lakini wanachosubiri ni kupatikana kwa mkandarasi atakayepitishwa baada ya tenda kutangazwa na halmashauri.

“Naamini tukifanya hivi mkandarasi akipatikana tunaweza kuujenga mradi huu ndani ya miezi minne bila wasiwasi wowote na tayari h1.5 bilioni zimetengwa kwa ajili kuutekeleza na shida ya maji katika eneo hili itakuwa historia,” amesema Profesa Mbarawa.

“kuna vyanzo vingi vya maji lakini miundombinu ya maji iliyopo katika eneo hili ni ya Zaidi ya miaka 30 hivyo inahitaji maboresho ili kuweka uhakika wa maji,”

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz