Jumla ya miradi mbalimbali ya Maendeleo 37 yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 37.9 inatarajiwa kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Tabora zinazoanza Julai 13,2021, huku Serikali ikiwa imechangia 35.7, Halmashauri zimechangia milioni 963, wananchi wamechangia milioni 142.
Kauli hiyo imetolewa leo Julai 12, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake, ambapo amesema kuwa ujumbe mkuu wa Mbio hizo Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 ni “TEHAMA ni msingi wa taifa endelevu; itumie kwa usahihi na uwajibikaji”.
Familia 300 za polisi kufaidika makazi ya kisasaAidha RC Dkt. Batilda amewaomba wananchi wote wa Mkoa huo kujitokeza na kushiriki mahali ambapo Mwenge wa Uhuru utapita na kushuhudia jitihada za Maendeleo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Sambamba na hayo RC Batilda amewakumbusha wakazi wa Mkoa wa Tabora kuendelea kuchukua tahadhari kubwa kwa Ugonjwa wa COVID 19 katika maeneo na shughuli zote za Mwenge wa Uhuru na Vitakasa mikono(Sanitizer), kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka.
Wanaozusha taarifa hizi wakamatwe – Rais MuseveniWananchi waonywa matumizi mabaya ya ardhi